NATEMBEYA APATA PIGO TRANS NZOIA MIKONONI MWA UDA.

Na Benson Aswani
Zaidi wa wafuasi 500 waliokuwa wakimpigia debe mshirikishi wa bonde la Ufa George Natemebeya kugombea wa kiti cha ugavana Katika Kaunti ya Trans-Nzoia wamehamia mrengo wa Mshauri mkuu wa miundo msingi na Teknolojia katika afisi ya Naibu wa Rais Maurice Kakai Bisau ambaye ametangaza kuwania kiti hicho kupitia kwa chama cha UDA.
Wakihutubia wanahabari eneo la Birunda eneo bunge la Saboti Kaunti ya Trans-Nzoia wafuasi hao wakiongozwa na Jeff Yabuna, Milton Waswa na Elizabetha Makokha wamesema wamechukua hatua hiyo baada ya tathmini ya kina kuhusu manifesto ya viongozi hao wawili mbali na uongozi wa chama cha UDA.
Kwa upande wake Kakai Bisau amepongeza Hatua ya wanachama hao, akipigia debe mfumo wa kiuchumi wa chama cha UDA wa Bottom Up economy akisema akiwa Gavana wa pili wa Kaunti ya Trans-Nzoia, atatenga zaidi ya shilingi milioni 200 zitakazotumika kuwapiga jeki wafanyabishara wadogo wadogo ikiwa ni pamoja na vijana wa bodaboda na mama mboga.