NATEMBEYA AONA MASHIRIKA YA MISAADA DHIDI YA KUINGIA TIATI KAUNTI YA BARINGO

Mshirikishi wa usalama kanda ya bonde la ufa George Natembeya amesema hakuna mashirika ya kutoa misaada ya kiutu yatakayoruhusiwa kuingia eneo la Tiati katika kaunti ya Baringo bila kibali.
Natembeya amesema kuwa wanaoingia eneo hilo ambalo si salama kwa sasa wanahatarisha maisha yao na hata wale ambao wanalengwa kwa misaada hiyo.
Serikali ilirejelea oparesheni ya kutwaa silaha zinazomilikiwa na wakazi wa eneo hilo kinyume cha sheria kwa kile ambacho kilitajwa kuwa kuongezeka utovu wa usalama baada ya serikali kuisitisha awali ili kutoa nafasi kwa viongozi kutoka kaunti hiyo na kaunti hii ya Pokot magharibi kupata mwafaka kupitia mazungumzo.
Seneta wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Samwel Poghisio alilalamikia hatua hiyo akisema kuwa muda waliopewa kuandaa mazungumzo na wakazi wa baringo haukuwa umekamilika.

[wp_radio_player]