NATEMBEYA AKANA KUWEPO NJAMA YA KUWAFURUSHA WAKAAZI KATIKA MASHAMBA YA KITALALE.


Aliyekuwa mshirikishi wa eneo la bonde la ufa ambaye pia anawania kiti cha ugavana kaunti ya Trans nzoia George Natembeya amejitenga na madai kwamba yuko na njama ya kuwafurusha wakazi wa Kitale na maeneo mengine iwapo atachaguliwa kuwa gavana wa kaunti hiyo.
Akizungumza mjini kitale baada ya kukutana na viongozi kutoka jamii ya wasabaot, Natembeya aidha amejitenga na madai kuwa atawafurusha wakazi wanaoishi eneo la msitu la Kitalale akisema wanaoeneza madai hayo wana nia ya kuwadanganya wakazi uchaguzi mkuu wa mwezi agosti unapokaribia.
Wakati uo huo Natembeya amekanusha madai kuwa alihusika katika kuwaondoa wakazi waliokuwa wamevamia msitu wa Mau akisema alikuwa akitekeleza maagizo kutoka kwa serikali ya kitaifa.
Amewahimiza wakazi kuishi kwa amani bila kutenganishwa na wanasiasa ambao wanaeneza jumbe za chuki kwa minajili ya kuzua vurugu wakati wa uchaguzi.