NASOKOL YAZURU MAKAO YA WATOTO YA SUNFLOWER.

Na Benson Aswani
Shule ya wasichana ya Nasokol kaunti hii ya Pokot magharibi Kupitia klabu ya Charity wameyatembelea jana makao ya watoto ya Sunflower na kutoa msaada wa bidhaa za msingi kwa ajili ya watoto hao.
Msimamizi wa klabu hiyo ambaye pia ni mwalimu katika shule hiyo ya Nasokol Milicent Mirikwa amesema kuwa lengo kuu la kuyazuru makao hayo lilikuwa kuwafanya watoto hao kuhisi kuwa wapo watu ambao wanawajali na pia kuwa wana haki kama vile watoto wengine.
Ni kauli ambayo imetiliwa mkazo na mwanachama wa klabu hiyo mwanafunzi wa shule ya Nasokol Noela Wekesa ambaye amesema waliamua kubuni klabu hiyo ili kuwasaidia hasa watoto mayatima ambao kulingana naye hupitia changamoto nyingi.
Meneja wa makao hayo Debora Nilson amepongeza shule hiyo kwa kujitolea kuwasaidia watoto hao huku akitoa wito kwa wahisani zaidi kujitokeza ili kuhakikisha kuwa watoto hao wanapata msaada ambao unastahili maishani na pia kuhisi kuwa kuna mtu anayewajali.