NANOK APUUZA RIPOTI ZA KUWEPO BAA LA NJAA TURKANA.

Na Benson Aswani
Gavana wa kaunti ya Turkana Josephat Nanok amepuuzilia mbali ripoti ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa baa la njaa linakumba kaunti ya Turkana na kuwa familia nyingi zinakosa chakula na sasa zinahitaji msaada wa dharura.
Nanok amesema kuwa ripoti hizo zimetiliwa chumvi na kuwa kaunti ya Turkana chini ya utawala wake imajipanga vilivyo kukabili baa la njaa.
Akizungumza na wanahabari katika afisi yake, Nanok amesema kuwa serikali yake imeweka mikakati ya kutosha kuhakikisha wakazi wa kaunti hiyo pamoja na mifugo hawajaathirika kufuatia ukame.