NAIBU WA RAIS WILIAM RUTO ANATARAJIWA KUZURU KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Mwaniaji urais wa chama cha UDA William Ruto anatarajiwa leo kuzuru kaunti hii ya Pokot maghari kuongoza kampeni za muungano wa Kenya kwanza katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wakazi.
Ziara ya Ruto inajiri siku chache tu baada ya mgombea urais wa chama cha muungano wa azimio la umoja one Kenya Raila odinga kuandaa kampeni zake kaunti hii ambapo alikita kambi eneo la Chepareria.
Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye ni mwandani wa Ruto amewataka wakazi katika kaunti hii kuhakikisha kuwa utulivu unadumishwa licha ya tofauti za kisiasa na kumpa nafasi Ruto kuuza sera zake.
Moroto ametumia fursa hiyo kushutumu vurugu ambazo zilishuhudiwa eneo la Tiati kaunti ya Baringo wakati wa ziara ya Raila Odinga huku akiwataka vijana kutokubali kutumika vibaya kisiasa na badala yake kuheshimu kila kiongozi nchini.