MWANGA WA TUMAINI KWA MWANAFUNZI AMBAYE NUSRA AKATIZE NDOTO YAKE.

Siku chache tu baada ya kituo hiki kuangazia masaibu yaliyomkabili mtahiniwa mmoja wa darasa la nane kutoka mtaa wa mawingo road viungani mwa mjini wa makutano Brian Kemboi ambaye alikuwa nusra akatize masomo yake ya shule ya upili kutokana changamoto ya karo na mahitaji mengine, hatimaye amejiunga na kidato cha kwanza.
Mhisani kwa jina Everlyne Rono ambaye amemsajili mwanafunzi huyo katika shule ya upili ya Mnagei amesema kuwa Juhudi hizo zimefanikishwa kupitia msaada kutoka kwa wahisani wengine ambao walishirikiana naye kuhakikisha mwanafunzi huyo anaendeleza masomo yake na kuafikia ndoto yake maishani.
Ametoa wito kwa wahisani zaidi kujitokeza katika kuhakikisha mwanafunzi huyo anakamilisha masomo yake bila tatizo huku akipongeza kituo hiki kwa kuangazia hatma ya mwanafunzi huyo ambaye alizoa alama 303 katika mtihani wa KCPE.