MWANAYE KIPNG’OK AIDHINISHWA RASMI NAIBU GAVANA WA BARINGO.

Bunge la kaunti ya Baringo limeidhinisha uteuzi rasmi wa Felix kiplagat maiyo kama naibu gavana kaunti hiyo kama ilivyopendeleza kamati ya uteuzi ya bunge hilo.

Kwenye kikao kilichoandaliwa mapema alhamisi wawakilishi wadi kwa kauli moja waliunga mkono uteuzi wa Kiplagat ambaye sasa atajaza nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha babake Charles Kipng’ok mwezi uliopita.

Kabla ya kuidhinisha ripoti hiyo wawakilishi wadi walikuwa na fursa ya kutoa maoni na mchango wao kuhusiana na utezu wa Kiplagat ambaye sasa anasubiri kuapishwa.

Aidha akitoa hoja zake mbele ya bunge hilo kiongozi wa wengi Lawi Kipchumba alisema kuwa Kiplagat alikuwa na ufahamu wa maswala mengi katika kaunti hiyo wakati alipokuwa akihojiwa.

Naibu gavana wa kaunti hiyo Charles Kipng’ok aliaga dunia  mwezi septemba wiki tatu tu baada ya kuchaguliwa katika uwanja wa ndege wa JKIA akijiandaa kuelekea jijini Mombasa kwa kongamano la magavana na manaibu wao.