MWANARIADHA HOSEA MWOK KUZIKWA LEO MURKWIJIT.


Mwanariadha anayedaiwa kujitia kitanzi katika eneo la murkwijit kaunti hii ya pokot magharibi Hosea Mwok anazikwa leo.
Mwili wa Mwok ulipatikana ukining’inia kwa kamba katika ghala la kuhifadhi chakula cha mifugo nyumbani kwake jumamosi iliyopita japo kufikia sasa chanzo cha kifo chake hakijabainika.
Hata hivyo baadhi ya wanaomfahamu wamesema kuwa alikuwa na msongo wa mawazo uliochangia matatizo ya akili kwa muda.
Hosea mwok alitamba zaidi katika mbio za mita alfu kumi na mbio za nyika kati ya mwaka 2004 na mwaka 2012 na aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 35.
Mazishi ya Mwok yanajiri wakati ambapo uchunguzi wa kifo cha mwanariadha mweza Agnes Tirop unaendelea.
Tayari imedaiwa kuwa mmewe Tirop alikuwa amewapigia simu wakwe zake akijutia alichokuwa amefanya japo hakukiri moja kwa moja kuwa alikuwa amemuua Tirop ambaye mwili wake ulipatikana chumbani ukiwa na majeraha ya kisu.