MWANAMMKE ALIYEFUNGA HARUSI NA ROHO MTAKATIFU KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AANZA UTUMISHI RASMI


Mwanamke aliyefunga harusi na Roho Mtakatifu katika Kaunti ya Pokot Magharibi wiki iliyopita Elizabeth Nalem ameanza rasmi utumishi wake kwa Mungu huku akisema ameagizwa kuzunguka dunia nzima.
Akizungumza na wanahabari katika eneo la Kanyang’areng’ alipokuwa akiingia nchini Uganda, Nalem amesema wanawe sita pamoja na mumewe watabaki nchini Kenya salama mikononi mwa Mungu huku utumishi wake ukianzia nchini Uganda na kuutamatishia mjini Jerusalem alikozaliwa Yesu Kristu.
Ikumbukwe Nalem na mumewe walikuwa wzmetofautiana vikali kuhusiana na wito huo hali iliyomsababishia mtumishi huyo wa Mungu kutoroka nyumbani kabla ya kufanikisha sherehe yake ya harusi baina yake na Roho Mtakatifu, hafla iliyohudhuriwa na wakazi wengi waliobaki na mshangao kuihusu.