MWANAMME MMOJA KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI AUAWA KWA KUDUNGWA KISU NA WATU WASIOJULIKANA


Maafisa wa polisi wanaendeleza msako wa washukiwa wa mauaji ya mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka hamsini na minane katika Lokesheni ya Chebor kwenye kaunti ya Pokot Magharibi.
Kulingana na Kamanda wa polisi wa kaunti hii Jackson Tumwet, mwendazake kwa jina Simkou Simon aliuwawa kwa kudungwa kisu mwilini mara tatu usiku na watu wanaoshukiwa kuwa ni wanawe wawili wakishirikiana na mama yao na kutoroka baada ya kutekeleza uhalifu huo.
Amesema marahemu alipatikana kwenye chumba chake cha kulala kabla mwanawe mdogo kuwaita majirani ambao baadaye waliwaarifu maafisa wa polisi kufika kwenye tukio.
Kulingana na Chifu wa Lokesheni hiyo Atudonyang’ Chebon, huenda mauji hayo yamesababishwa na migogoro ya kifamilia ambayo familia hiyo imeshuhudia tangu mwendazake alipooa mke wa pili.
Amesema miongoni mwa washukiwa wa mauaji hayo ni mwanafunzi wa kidato cha nne.