MWANAMME MMOJA ENEO LA MACHEWA BONDENI KAUNTI YA TRANSNZOIA AMEMKATA MAMAKE KWA UPANGA NA KISHA KUUWAWA NA WAKAAZI WENYE HAMAKI.
NA BENSON ASWANI
Mwanamme mmoja mwenye Umri wa miaka Hamsini na Mitatu Mkaazi wa Bondeni Machewa katika kaunti ya Transnzoia amemuuwa Mamake mwenye umri wa miaka Sabini na sita kwa kumkata kwa upanga kufuatia mzozo wa kinyumbani
Kwa mjibu wa Ndugu zake Chemos Mneria na Vincent Mneria mwenda zake Alfred Boiyo alikerwa na hatua ya mamake kumtenganisha wakati alipokuwa akimpiga mkewe fridah naliaka.
Mke wake Fridah Naliaka ameiambia Kalya radio kwamba mumewe Boiyo alipandwa na Hasira alipomrai kuacha kumwadhibu Binti wao wa Gredi ya tatu kutokana na Rekodi duni katika Mtihani wake.
Mwili wa Mama huyo umeifadhiwa katika Chumba cha Maiti cha Kiminini Cottage.
Hata hivyo Mwili wa Mwanaumme huyo ambaye baadaye alivamiwa na umati wenye gadhabu na kuuliwa pia ulihifadhiwa katika chumba cha maiti cha Cottage kiminini.