MWANAMME MMOJA APATIKANA NA BASTOLA BILA RISASI LIKUYANI


Maafisa wa Polisi katika kaunti ndogo ya likuyani wanamzuilia mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na minne baada ya kupatikana na bastola katika kijiji cha kongoni.
Akidhibitisha kisa hiki kinara wa polisi katika eneo hilo Charles Muthuye amesema baada ya kupokea fununu kutoka kwa wananchi maafisa wa polisi walifanya msako katika nyumba ya mshukiwa Kelvin Shivachi ambapo walifanikiwa kuipata hiyo iliyokuwa imefichwa chini ya Godoro kwenye kitanda chake
Muthuye amesema walifanikiwa kumnasa mshukiwa ambaye kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Nangili akisubiri kufikishwa mahakamani hii leo akihoji kuwa bastola hiyo haikuwa na risasi.
Kisa hiki kinajiri baada ya wakaazi wa eneo hili kulalamikia kukithiri kwa visa vya uhalifu wakihoji kuvamiwa kuporwa mchana peupe na kundi la vijana wanaotumia Pikipiki isiokuwa na nambari ya usajili