MWANAMME MMOJA ANASAKWA BAADA YA KUOA MSICHANA WA MIAKA KUMI NA TATU KACHELIBA POKOT MAGHARIBI

Mwanamme mwenye umri wa makamu anatafutwa na Polisi Katika Eneo la Kacheliba baada ya kuoa msichana mwenye umri wa miaka kumi na mitatu katika Kijiji cha Koroa kwenye Wadi ya Suam na kulipa mahari ya ng’ombe ishirini.

Kulingana na Chifu wa Suam Shaban Akida, msichana huyo aliripoti kisa hicho katika Kituo Cha Kacheliba ambako anazuiliwa huku wazazi wake na aliyemwoa wakitafutwa baada ya kuingia mafichoni.

Akida amesema wapo wasichana wengine watatu ambao wamenusuriwa baada ya kuoleka na kupelekwa kwenye taasisi za Kiufundi.

Amesema kwamba ipo haja ya jamii kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa elimu ya wanao akiwaonya vikali watakaopatikana wakioza mabinti zao.