MWANAMME MMOJA AMWIBA MBUZI WA JIRANI NA KUMCHINJA ITEN

ELGEYO MARAKWET


Mahakama ya Iten imemwamuru mwanamme mmoja katika eneo hilo kulipa shilingi alfu tatu ama kusalia korokoroni kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kupatikana na mbuzi wa wizi.
Mahakama hiyo ilieleza kuwa tarehe mosi mwezi huu wa Disemba katika eneo la Rware eneobunge la Marakwet Magharibi katika kaunti ya Elgeyo Marakwet Edwin Kiprona aliiba mbuzi mwenya thamani ya shiliningi alfu tatu na miatano mali ya Oliver Kemboi.
Mshtakiwa alikabiliwa na shitaka la pili kwamba yeye pamoja mwengine ambaye hakuwa mahakamani walishirikiana kumwiba mbuzi huyo na kumficha kabla ya kumchinja.
Kiongozi wa mahakama Clare Kosgei aliielezea mahakama kwamba mlalamishi aliwafungua mbuzi wake kwenda malishoni saa mbili asubuhi kisha alipokwenda kuwaangalia saa saba mchana akagundua kuwa mmoja alikuwa ametoweka na baada ya kumtafuta kwa muda akapata mshukiwa akiwa katika harakati ya kumchinja mbuzi huyo.
Mshukiwa alikubali makosa hayo mbele ya hakimu mwandamizi Charles Kutwa na kuomba kusamehewa na mahakama. Hata hivyo mshukiwa ako huru kukata rufaa ndani ya siku kumi na nne.