MWANAMME AJITIA KITANZI KAKAMEGA BAADA YA KUMPATA MKEWE AKIONGEA NA MWANAMME MWINGINE


Hali ya majonzi imetanda katika kijiji cha Shikoti eneo bunge la Llurambi kaunti ya Kakamega baada ya mwanamme wa miaka 37 kwa jina Simon Akhonya kujitia kitanzi kwa madai kuwa alimpata mkewe akiongea na mpango wa kando nje ya nyumba yake nyakati za usiku.
Mamake marehemu Chrisine Awinja pamoja na wanafamilia wanasema mwendazake alidai kuwa aliporejea nyumbani alimfumania mkewe Elizabeth Kutekha, akila uroda na mwanamme huyo nje ya nyumba yake jambo lilopelekea kujitia kitanzi.
Familia ya mwendazake inadai marehemu na mkewe wamekuwa na ugomvi wa kila mara, huku mwili wake ukiondolewa na maafisa wa polisi na kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya kakamega kufanyiwa upasuaji.