MWANAMME AJITIA KITANZI BAADA YA KUBAINI KUWA ATAWEKEWA CHUMA KWENYE MGUU WAKE


Uchunguzi umeanzishwa kubaini kifo cha mwanamme mwenye umri wa miaka 38 ambaye mwili wake umepatikana nyumbani kwake katika kijiji cha Bulusu eneobunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega.
Mwanamme huyo alijitia kitanzi akitumia nyaya za kuanika nguo kwa madai kwamba jamii yake ilikuwa na mpango wa kumuwekea chuma kwenye mguu wake uliovunjika.
Kulingana na famila ya mwendazake ni kwamba marehemu alikuwa pia anazongwa na mawazo baada ya kubainika anaugua virusi vya HIV.