MWANAMME AIAGA DUNIA BAADA YA KUDUNGWA KISU MARA KADHAA BAADA YA KUTOFAUTIANA NA MWENZAKE KWA SABABU YA SALAMU


Mwanamme mmoja mkaazi wa kijiji cha Kapkonga kwenye eneobunge la Keiyo Kusini katika kaunti ya Elgeyo Marakwet ameuliwa kwa kudungwa kisu mara kadhaa baada ya kutofatiana vikali na mwezake kuhusu salamu.
Akidhibitisha kisa hiki chifu wa Kapkonga Philip Ruto amesema kwamba Allan Kiplagat mwenye umri wa miaka ishirini na miwili alidungwa kisu na mwenzake Leonard Koech mwenye umri wa miaka ishirini na sita alipomuita kijana alipokuwa akimsalimia.
Ruto amesema baada ya mshukiwa kutekeleza kitendo hicho ametoweka na sasa anataftwa na maafisa wa polisi.
Hayo yanajiri saa chache tu baada ya mwanamme mmoja kwenye eneo la Kipsoen katika kaunti ndogo ya Keiyo Kusini kupatikana akiwa amejitia kitanzi baada ya mzozo wa familia kuzuka nyumbani.
Kwa mjibu wa chifu wa eneo hilo Richard Mutahi mwanamme huyo kwa jina John Kiplimo alipatikana akininginia kwenye mti uliokuwa karibu na boma lao.