MWANAMME AFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA UKUTA WA NYUMBA WADI YA KANAMKEMER KAUNTI YA TURKANA.


Mwanammwe mwenye umri wa makamo katika wadi ya Kanamkemer kaunti ya Turkana amethibitishwa kufariki baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba alipokuwa anaubomoa na mwenzake.
Kulingana na walioshuhudia tukio hilo wamesema kwamba marehemu alikuwa akibomoa ukuta huo kutoka chini badala ya kubomoa kutoka juu.
Hali hiyo imepelekea mmiliki wa kampuni moja ya ujenzi eneo hilo Felix Ojiambo amewataka wamiliki wa nyumba kwenye kaunit hiyo kuhakikisha kwamba wanazingatia usalama wa wafanyikazi wao.
Wakati uo huo Ojiambo amewataka mafundi kuvalia magwanda wakati wa ujenzi ili kuzuia maafa zaidi.