MWANAMKE ALIYEDAI KUFANYA HARUSI NA ‘ROHO MTAKATIFU’ AJIUZULU RASMI KAZI YAKE.


Elizabeth Nalem, mwanamke aliyejidai kufanya harusi na Roho Mtakatifu katika Kaunti ya Pokot Magharibi ameiacha kazi yake aliyokuwa akifanya katika kaunti na hata kufunga hoteli yake kwa madai ya kuitikia wito wa Mungu wa kuhubiri neno.
Nalem ambaye alisalia kimya kwa muda baada ya kukemewa na watu wengi kwa madai ya kupagawa, amedai kuwa Mungu amemwagiza kufungua Kanisa lake nyumbani kwake kwa jina Jesus Name.
Aliyekuwa msimamizi wake kwenye harusi aliyodai kufanya na Roho mtakatifu Lydia Madanyang’ amesema mambo yote wanayotenda na kote wanakoenda ni kwa agizo la Mwenyezi Mungu.