MWANAMKE AJILIPIA MAHARI KAKAMEGA.

Mwanamke mmoja kutoka kijiji cha shangazi kata ndogo ya marakusi kaunti ndogo ya lugari kaunti ya kakamega amewashangaza wakazi  baada ya kuwafungua  ng’ombe wawili wa mumewe zizini na kuwapeleka kwao kujilipia mahari.

Mmewe mwanamke huyo Augustine muhanji anasema mkewe ambaye wameishi naye kwa zaidi ya miaka 20 Caroline nang’onda simiyu na kujaliwa watoto watano, alifungua ng’ombe hao mmoja ambaye ni mjamzito na kuwapeleka nyumbani kwao kama mahari yaliyosalia.

Baba mkwe wa mshukiwa Nathan muhanji na nduguye linus atsango, wanadai hatua hiyo ni kinyume cha sheria za jamii ya luhyia kwani ni makosa kwa mshukiwa kufungua ng’ombe aliyekuwa na ndama tumboni na ni makosa kwa ng’ombe huyo kujifungua akiwa nyumbani kwao.

Walisema kile wanafahamu kijana yao alipeleka ng’ombe wawili kama  mahari na sasa walikuwa wakijipanga kumalizia mahari iliyosalia kinyume na jinsi alivyochukua uamuzi huo.