MWANAMKE AFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA MUME WAKE FIMBO KICHWANI


Mwanamke mmoja katika eneo la Sun Flower hapa mjini Makutano kaunti ya Pokot Magharibi amethibitishwa kuiaga dunia baada ya kupigwa na mume wake kichwani mara kadhaa akitumia fimbo usiku wa kuamkia leo.
Akithibitisha tukio hilo Mkuu wa polisi katika kaunti ndogo ya Pokot Magharibi Julius Chumbule amesema kuwa maafisa wa polisi walifanikiwa kufika kwenye tukio na kumtia mbaroni mshukiwa.
Inadaiwa kuwa wawili hao walizozana kutokana na mwanamme huyo kufika nyumbani kisha kumpata mke wake hayuko.
Kwa sasa mwanamme huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi huku akitarajiwa kufunguliwa mashtaka pindi tu uchunguzi utakapo kamilika huku mwili wa mwendazake ukihifadhiwa katika chumba cha wafu cha hospitali ya Kapenguria.