MWANAMKE ABAKWA NA KUULIWA MTAANI MATHARE MAKUTANO KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Mwanamke mmoja mama ya mtoto mmoja ameaga dunia baada ya kubakwa usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mathare viungani mwa mji wa Makutano kaunti hii ya Pokot Magharibi.
Ni kisa ambacho kimeshutumiwa vikali na wakazi wa kijiji hicho ambao wamesema kuwa kisa hicho si cha kwanza kutokea eneo hilo na kuwa hamna hatua yoyote ambayo imechukuliwa licha ya lalama zao za kila mara.
Wakazi hao wamesema kuwa visa hivyo vimechangiwa na kukithiri uvutaji wa bangi miongoni mwa vijana katika kijiji hicho pamoja na ugemaji wa pombe, wakishutumu maafisa wa polisi kwa kutochukua hatua kukabili ugemaji pombe eneo hilo.
Imewalazimu maafisa wa polisi kuingilia kati na kumwokoa mhusika kutokana na ghadhabu za wakazi huku mwili wa mwenda zake ukiondolewa eneo hilo.