MWANAKANDARASI ANAYEKARABATI BARABARA KADHAA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI ASHAURIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KIKAMILIFU


Mwanakandarasi aliyepewa jukumu la kukarabati barabara kadhaa eneo bunge la Kapenguria kaunti hii ya Pokot Magharibi ametakiwa kutekeleza kikamilifu majukumu yake.
Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto amesema mwanakandarasi huyo amezembea kazini kwani tangu alipokabidhiwa jukumu la kujenga barabara hizo hamna hatua zozote ambazo zimepigwa kufikia sasa.
Aidha Moroto amemshutumu mwenyekiti wa maswala ya ujenzi wa barabara nchini kwa kile amedai kuingilia shughuli za ujenzi wa barabara hizo akitishia huenda wakamchukulia hatua za kisheria.
Wakati ou huo Moroto ametoa wito wa kuimarishwa zaidi hali ya barabara zinazoelekea kwa baadhi ya shule eneo hili akisema kiasi kikubwa cha fedha kimetengewa shughuli ya ujenzi wa barabara hizo.