MWANAFUNZI WA NASOKOL AIBUKA WA PILI KITAIFA KATIKA UANDISHI WA INSHA KWENYE ZOEZI LA SPELLING BEE.

Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Nasokol katika kaunti ya Pokot magharibi ameibuka wa pili nchini katika zoezi la uandishi wa insha maarufu spelling bee ambalo lilifadhiliwa na kampuni ya pwani oil.

Mwalimu mkuu was shule hiyo Cecilia Ngige alisema kwamba wanafunzi watano wa shule hiyo walishiriki zoezi hilo na kuibuka washindi katikakiwango cha kaunti kabla ya kuchujwa na kusalia wawili katika kiwango Cha kitaifa ambapo Joel Chelot aliibuka wa pili kitaifa.

Chelot Sasa anatarajiwa kuelekea jijini Mombasa kutuzwa na waziri wa elimu Ezekiel Machogu.

Ngige aliwahimiza wanafunzi zaidi katika kaunti hiyo kushiriki zoezi hilo katika siku za usoni ili kuinua jina la kaunti ya Pokot magharibi na kubadili dhana ambayo imekuwepo kwa miaka mingi kuhusiana hali ya elimu kaunti hiyo.

“Tulikuwa na mashindano ya kuandika insha kwa kiingereza ambayo yalijumuisha kaunti zote. Baadhi ya wanafunzi wangu walihusika ambapo watano waliibuka bora kaunti hii, huku mmoja akiibuka wa pili kitaifa. Hatua hii imetufurahisha na ni ufanisi mkubwa sana kama shule.” Alisema Ngige.

Akielezea ushindi wake Chelot alisema ameridhika kuona kwamba aniweka shule yake katika ramani ya taifa kielimu na kuwahimiza wanafunzi wenzake kushiriki zoezi hilo katika siku za usoni.

“Sikutarajia kuibuka wa pili Kenya nzima. Nafurahia sana kwamba nimewakilisha vyema shule yangu na kaunti ya Pokot magharibi kwa jumla. Nawaomba wanafunzi wenzangu kushiriki mazoezi haya kwani ni muhimu sana.” Alisema Chelot.