MWANAFUNZI WA GREDI YA NNE AWACHA MASOMO KUSHUGHULIKIA MAMAKE NA WADOGO WAKE KAPSOWAR

ELGEYO MARAKWET


Mwanafunzi mmoja wa gredi ya nne kwenye shule ya msingi ya kapsowar katika kaunti ya Elgeyo Marakwet amelazimika kukatiza masomo yake ilikukithi mahitaji ya malezi ya nduguze pamoja na mamaye aliyelazwa katika hospitali ya misheni ya kapsowar kutokana na maradhi ambayo yamemsababishia kiharusi.
Mvulana huyo mwenye umri wa kumi na wawili pekee anategemea pakubwa biashara ya kutafta kuni na kuuza ilikukithi mahitaji ya familia yao.
Brian Kiplagat licha ya umri wake mdogo amelazimika kuishi na kakaye mwenye umri wa miaka misaba na dadaye mwenye umri wa miaka mitatu baada ya mamayao kulazwa hospitalini kwa miezi mitano sasa.
kutokana na hali umasikini brian anategemea kuni anazotafta msituni na visazo vya makaa ambavyo huwa anauzwa angalau apate pesa za kununua chakula.
Vilevile Brian anajukumu la kumtembelea mamaye Filaris Kemboi hospitalini ambaye anamatatizo ya tumbo na mguu wake wa kushoto umepooza kutokana na kiharusi hali hii inamtia filaris wasiwasi na mguu wake umepooza kutokana na kiharusi hali hii inampa wasiwasi pia kumpa msongo wa mawazo ikizingatiwa kuwa kwa miezi tano hajafanikiwa kupata fedha za kugharamia matibabu bora na kujumuika na wanawe nyumbani.
Familia ya Brian sasa inaomba wakenya walio na uwezo kujitokeza kusaidia ilimamaye apate kuhudumiwa arejeee shuleni kuendelea na masomo yake.