MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO AJITIA KITANZI

KAKAMEGA


Mwanafunzi mmoja wa darasa la tano amejitia kitanzi ndani ya jikoni ya ya wazazi wake katika kijiji cha Eshurumbwe katika eneo bunge la Matungu kwenye kaunti ya Kakamega.
Familia yake marehemu ikiongozwa na babake John Otieno inasema walipata kijikaratasi ndani ya mfuko wa mwendezake akisema aliamua kujitoa uhai kwa madai ya kushinikizwa na wazazi wake kurejea shuleni ilhali amekuwa akijitegemea kupitia vibarua akipata pesa za kujiendeleza.