MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA AUWAWA CHUMBANI MWAO LIKUYANI KAKAMEGA


Wimbi la simanzi limetanda katika kijiji cha kilimani kata ya Likuyani kwenye kaunty ya Kakamega baada ya mtoto mmoja mwenye umri wa miaka kumi na minne kuuwawa kinyama na Maiti yake kufungwa ndani ya nyumba ya babuye kijijini humo.
Kulingana na Babuye Mwendazake mzee Binaiza Kidavi ambaye huishi jijini Nairobi mtoto huyo ambaye ni Mwanafunzi wa Darasa la saba katika shule ya msingi ya Kambi Mapesa amekuwa akiishi Bomani humo pekee yake kabla ya kuuwawa na Watu wasiojulikana.
Mzee Kidavi amesema tangu tarehe ishirini na tatu amekuwa akijaribu kumtafta Mjukuu wake kupitia Rununu bila ya mafanikio kabla ya kuamua kusafiri hadi nyumbani usiku wa kuamkia hiyo jana ambapo aliupata mlango ukiwa umefungwa kwa nje kwa Kufuli na ikamlazimu kuuvunja kabla ya kukumbana na maiti ya mjukuwe iliyokuwa na majeraha mabaya ikionzea ndani ya nyumba yake.
Maiti hiyo iliondolewa na Maafisa wa polisi kutoka kituo cha Turbo na kupelekwa katika hifadhi ya wafu ya Hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret huku uchunguzi ukianzishwa kuhusiana na kisa hicho.
Kisa hiki kimedhibitishwa na Kaimu Chifu wa kata ya Likuyani Peter Lugano.