MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA AONYESHA UELEDI WAKE KWA KUUNDA DRONI MJINI KITALE KAUNTI YA TRANSNZOIA


Mwanafunzi mmoja wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Chepkoilel Birunda, kwenye kaunti ya Trans nzoia ametengeneza droni kwa kutumia vifaa vya plastiki, mabati na nyaya kuu kuu.
Mwanafunzi huyo anasema kwamba kilichomchochea kutengeneza droni yake ni kutokana na kushuhudia droni zikitumika katika hafla za arusi na sherehe nyingine kuchukua picha na video.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Masia Butaki amesema kwamba usimamizi wa shule hiyo umekuwa ukifuatilia kipaji chake kwa muda mrefu akijihusisha na ufundi wa vifaa mbalimbali vya kielektroniki.