MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU KAKAMEGA AUWAWA.
Maafisa wa Polisi Wameanzisha Uchunguzi kuhusiana Mauaji ya Mwanafunzi wa mwaka wa Nne anayesomea taaluma ya uhandisi katika Chuo kikuu cha Masinde Muliro kaunti ya kakamega.
Wakaazi wakiongozwa na Cornelius Chemwali wanasema Marehemu Jonathan Telewa alifumaniwa na watu wawili waliokuwa wamevalia Kofia na kufunika Nyuso zao na kumpokonya Simu ya Rununu msichana aliyekuwa naye wakielekea katika makaazi yao Mtaa wa Lurambi karibu na Msitu wa kakamega
Na wakati marehemu alijaribu kuwazuia vilevile wakampora simu na Kumduga kwa Kisu mara kadhaa kifuani kisha wakatoweka
Kaimu Ocpd wa kakamega Daniel Mkumbu amesema Maafisa wake wameanzisha Uchunguzi wa kina kuhusiana na mauaji hayo ya kinyama akiwataka wanafunzi na usimamizi wa chuo hicho kuwa na subira.