MWANAFUNZI WA CHUO CHA KIBABII ALIYEPIGWA RISASI MARA NNE AZIKWA KWAO NAMANJALALA

TRANS NZOIA


Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kibabii Sabatian Wanjala Simiyu aliyeuliwa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi majira ya alfajiri anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao kwenye kijiji cha Namanjalala katika kaunty ya transnzoia huku hisia kali zikitarajiwa kutolewa kushinikiza haki kutendewa familia iliyofiwa
Msemaji wa familia hiyo ambaye vilevile ni kakake Michael Wekesa amesema kwamba utaratibu uliowekwa na wizara ya afya na shirika la afya duniani WHO utazingatiwa wakati wa mazishi hayo
Wekesa bila kuangazia kwa udani amesema kwamba ripoti ya upasuaji ulioendeshwa na dkt wa ubinafsi aliyefadhiliwa na mashirika ya umma unaonyesha kwamba Sebastian aliuliwa kwa kupigwa risasi mara nne.
jana jioni msafara mrefu ulishuhudiwa wakati wa kuondolewa kwa mwili wake kutoka hifadhi ya maiti ya hospitali level 4 mjini kitale ukisafirisha kuenda nyumbani
Tayari maafisa wa tume ya kutathimini utendakazi wa polisi ipoa na kituo cha haki na amani wamezuru boma la mwendazake na kurekodi taarifa huku afisa anayetuhumiwa kutekeleza mauaji hayo akisalia kuwa huru
hata hivyo kamanda wa polisi wa kaunty hiyo fredrick ochieng amesema kwamba idara ya upelelezi DCI inaendeleza uchunguzi wake kuhusu kisa hicho na kwamba afisa atakayepatikana akitumia nguvu kupita kiasi atachukuliwa hatua kali za kisheria.