MWANAFUNZI MMOJA ALIYEZOA ALAMA YA 303 KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AKOSA KARO YA KUJIUNGA NA SHULE YA UPILI


Mtahiniwa mmoja aliyefanya mtihani wa darasa la nane KCPE mwaka 2021 katika kaunti hii ya Pokot magharibi ametoa wito kwa wahisani kujitokeza ili kumsaidia kufanikisha elimu yake ya shule ya upili.
Brian Kemboi mkazi wa mawingo road viungani mwa mji wa makutano na ambaye alipata alama 303 katika mtihani wa KCPE na kutengewa nafasi katika shule ya upili ya wavulana ya Kamito,amesema kuwa amekuwa akisaidiwa na shule Pamoja na majirani zake kutokana na hali ya umasikini ya familia yake.
Ni wito ambao umekaririwa na mamake mwanafunzi huyo Lorna Chebet ambaye amesema kuwa amepitia wakati mgumu kuwalea wanawe kutokana na kutokuwa na chanzo muhimu cha fedha za kuweza kuwashughulikia.
Majirani wa familia hiyo wakiongozwa na Jennifer Ekalale wameelezea hofu ya mwanafunzi huyo kupotoka iwapo hatasaidiwa kuendeleza masomo yake wakiomba wahisani kumsaidia ili kuafikia ndoto ya kemaishani.