MWANAFUNZI ATEMBEA KILOMITA 50 KUSAJILIWA KATIKA SHULE YA UPILI TRANS NZOIA.


Usajili wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza ukiingia siku ya pili hii leo, mwanafunzi mmoja amelazimika kutembea kilomita 50 ili kujiunga na shule ya upili ya wavulana ya kitaifa ya st joseph mjini kitale kaunti ya Trans nzoia huku akifika bila chochote.
George masinde anadai aliamua kuchukua hatua hio baada ya kuarifwa na majirani zake kuwa siku ya leo ilikua ya mwisho wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza.
Ilimubidi mamake Damaris Mutenyo kumufuata hadi shuleni humo huku akiwataka wahisani kumsaidia mwanawe kwani yeye hana uwezo wa kugharamia karo katika shule hiyo kutokana na kipato chake cha chini.
Mkuu wa shule hiyo Godfrey Owuor ametaka wahisani kumsaidia akisema hatomtimua kutoka shuleni kwa kuonyesha nia yake ya masomo.