MWALIMU MMOJA AJINYONGA BAADA YA KUSONGWA NA MAWAZO YA MADENI CHEPARERIA

POKOT MAGHARIBI


Hali ya simanzi imegubika shule ya upili ya kalya uko chepareria eneobunge la Pokot kusini ni baada ya mwalimu mmoja kujitia kitanzi nyumbani kwake asubuhi ya leo.
Duru za kuaminika zinasema kwamba Mwalimu huyo amejitia kitanzi kutokana na deni kubwa alilochukua katika matawi tofauti ya benki nchini na kufikisha idadi kubwa ya deni.
Kando deni hilo kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya kalya mwalimu huyo kwa jina Lucy chebeti alikuwa amewasilisha tena stakabadhi zingine kwa afisi ya mwalimu huyo mkuu ili atie saini tena kuagiza mkopo mwingine hiyo juma lililopita
Kalyaradio imebaini kwamba mwalimu mwendazake Lucy chebeti alikuwa na mzozo wa mara kwa mara na mumewe ambaye amekuwa akichukua hela zake kila wakati pasi na kumwarifu mahala anakopeleka hela hizo ikizingatiwa bi Lucy alikuwa amefungua biashara katika soko la chepareria.
Kwa sasa maafisa wa polisi wameuchukua mwili wa mwendazake na kupelekwa katika chumba cha wafu katika hospitali ya rufaa ya kapenguria.