MWALIMU AKUNG’UTWA NA WANAFUNZI SABOTI TRANS NZOIA.
Mwalimu mmoja wa shule ya upili ya mseto ya Nakuto st Johns Sikinwa kwenye eneo bunge la Saboti kaunti ya Trans nzopia amerekodi taarifa baada ya kushambuliwa na watahiniwa wake watatu kwa vifaa butu huku walimu wengine wawili wakiponea.
Nicholas Bett mwalimu wa somo la fizikia na hisabati amesema kuwa watahiniwa hao walimkabili nyumbani kwake saa moja usiku siku ya jumaosi na kumpiga vibaya.
Walimu wengine wawili walioponea katika kisa hicho John Naibei na Michael Odhiambo waliandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Gituamba wakitaka wanafunzi hao kukamatwa na kuhukumiwa mahakamani.
Wanafunzi hao walitoweka baada ya kitendo hicho na hawajaripoti shuleni kuanzia siku ya jumatatu juma hili.
Chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET tawi la Trans nzoia kupitia katibu wake Furaha Lusweti sasa kitaitaka tume ya huduma za walimu TSC kuwapa uhamisho walimu hao watatu ambao walikuwa wamelengwa.