MWAKILISHI WADI YA LELAN POKOT MAGHARIBI AENDELEA KUOMBOLEZWA.

Viongozi katika kaunti hii ya Pokot Magharibi wameendelea kumwomboleza mwakilishi wadi ya Lelan Johnson Lokato.
Wa hivi punde kumwomboleza Lokato ni mgombea kiti cha ubunge eneo la Pokot kusini James Teko ambaye amesema kuwa kaunti hii imempoteza kiongozi shupavu ambaye alikuwa msitari wa mbele katika kupigania maswala ya amani.
Teko amesema kuwa kaunti hii imepata pigo kubwa kufuatia kifo chake Lokato huku akiitakia makiwa familia ya mwenda zake.
Aidha Teko amesema huu ni wakati mgumu kwa kaunti hii hasa ikizingatiwa katika kipindi kifupi zaidi imewapoteza waakilishi wadi wawili mfululizo.