MWAKILISHI WA AKINA MAMA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AWATAKA WANASIASA KUFANYA SIASA KOMAVU


Wanasiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuenedelza siasa komavu na kujitenga na kutumia majukwaa ya kisiasa kuelekeza cheche za maneno kwa wapinzani wao.
Ni wito wake mwakilishi kina mama katika kaunti hii Lilian Tomitom ambaye amewasuta baadhi ya wapinzani wake kwenye wadhifa huo kwa kile amesema kuwa kutumia jina lake kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wapiga kura.
Tomitom ambaye anatetea kiti hicho kupitia tiketi ya chama Cha UDA, amewataka wanasiasa kujitenga na siasa za kuharibiana majina na badala yake kutafuta kura kwa kuuza sera zao kwa wananchi ambao amesema watawachagua viongozi kulingana na sera zao.
Aidha Tomitom ametumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa kaunti hii kumchagua tena katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti ili kukamilisha aliyoanzisha katika muhula wake wa kwanza kama mwakilishi kina mama katika kaunti hii ya Pokot magharibi.

[wp_radio_player]