MVULANA MMOJA MLEMAVU ANAUGUZA MAJERAHA MABAYA KATIKA HOSPITALI YA KAPENGURIA BAADA YA KUPIGWA RISASI KWENYE MAPAJA .


NA BENSON ASWANI
Mvulana mmoja wa miaka kumi na tisa ambaye ni Mlemavu kutoka lokesheni ya Chesogon kaunti ya Pokot Magharibi anauguza majeraha mabaya ya hospitali kuu ya rufaa ya kapenguria baada ya kupigwa Risasi na wavamizi wa eneo hilo wanaokisiwa kuwa wezi wa Mifugo ambao walifaulu kukwepa na mbuzi kumi na nne.
Baada ya wakaazi wa eneo hilo kulalamikia usalama katika eneo hilo kuwa umedorora zaidi
Kwa mjibu wa nduguye Stephen Losia mwathiriwa kwa jina Piu Losia alikumbana na wavamizi hao waliokuwa wamejihami kwa Bunduki na walianza kufyetua Risasi kiholela huku wakimjeruhi mwathiriwa kwa kumpiga kwenye mapaja yake yote mawili
Ukosefu wa maafisa wa usalama katika eneo hilo umetaja kuchangia pakubwa visa hivyo huku wakaazi wakishi kwa hofu kubwa ya kuvamiwa kila wakati
Akizungumza baada ya kuzuru Hospitali hiyo Gavana wa kaunti ya kaunti hii ya pokot magharibi John Lonyangapuo ameshtumu vikali kisa hicho na kusema kuwa ni swala la kusikitisha mno kuona watu waliojihami kwa Bunduki wakitembea kiholela na kusababisha maafa