MUUNGANO WA WANAFUNZI WATAKA SERIKALI KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILI UTOVU WA USALAMA BONDE LA KERIO.


Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka kaunti hii ya Pokot magharibi, wameitaka serikali kuweka mikakati ya kutosha itakayopelekea kukabiliwa hali ya utovu wa usalama katika eneo zima la bonde la Kerio.
Wakizungumza baada ya kikao na viongozi wa wanafunzi hao kutoka kaunti za Baringo, Elgeyo marakwet na Turkana, viongozi wa muungano huo wakiongozwa na Mathew Powon wamesema kuwa visa vya utovu wa usalama vimeathiri pakubwa sekta ya elimu na ni wakati suluhu ya kudumu inafaa kupatikana.
Aidha wameshutumu kisa cha wiki iliyopita ambapo basi la shule ya upili ya Tot katika kaunti ya Elgeyo marakwet lilivamiwa na kujeruhiwa wanafunzi 13 pamoja na walimu wawili huku dereva wa basi hilo akiuliwa.
Wakati uo huo wanafunzi hao wameitaka serikali kuwaunga mkono katika juhudi zao za kutafuta amani kupitia mkakati wao wa amani mashinani inniciative wakisema ndio walio katika nafasi bora ya kuhakikisha amani inaafikiwa maeneo haya.
Wamewataka pia wanasia kuendeleza siasa za amani na kutochochea visa vya utovu wa usalama maeneo haya.