MUSTAKABALI WA NPR WAENDELEA KUIBUA HISIA BONDE LA KERIO.
Hisia mbalimbali zinaendelea kutolewa kuhusiana na kauli ya Naibu wa Rais William Ruto ya kurejesha Askari wa Akiba waliofutwa kazi ikiwa ni mpango wake wa kuimarisha amani miongoni mwa jamii zinazozozana.
Wakizungumza na na vyombo vya habari eneo la Kacheliba katika kaunti hii ya Pokot magharibi wakiongozwa na Gabriel Lonyiko, baadhi ya wazee wa jamii ya Pokot wamekubaliana na kauli ya Ruto kwamba serikali iliondoa maafisa wa akiba NPR kwa lengo la kumharibia jina.
kwa upande wake Joseph Lobong’ amesema iwapo kutakuwa na haja ya kuwarejesha Askari wa Akiba, basi itakuwa vyema kuwapa silaha na kuwalipa vyema ili wasije wakapata majaribu ya kutumia silaha hizo kwa njia mbaya.
Hata hivyo, baadhi ya wazee hao wakiongozwa na Gabriel Lonyiko wamepinga kauli ya kuwarejesha akitaka serikali ijayo kuchukua jukumu la kuwapokonya raia silaha zote ambazo zinamilikiwa kinyume cha sheria na ambazo zinatumika na wahalifu.