MUNYA AZURU TRANS NZOIA KUZINDUA UUZAJI WA MBOLEA YA BEI NAFUU.


Waziri wa kilimo Peter Munya anazuru leo kaunti ya Trans nzoia kuzindua uuzaji wa mbolea ya bei nafuu siku chache tu baada ya kuitikia wito wa wakulima na kupunguza bei ya mbolea.
Munya anatarajiwa kuwasili mjini kitale leo na kufanya mkutano mfupi na viongozi pamoja na wadau mbali mbali wa kilimo kabla ya kueleka kwenye afisi za bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao NCPB mjini Kitale na kufanya mkutano kisha kuzindua uuzaji wa mbole hiyo.
Ni shughuli ambayo pia anatarajiwa kuifanya katika kaunti ya Uasin Gishu.
Tayari viongozi mbali mbali katika kaunti hiyo ya Trans nzoia wamemrai waziri huyo kuhakikisha kuwa mbolea hiyo inafikia wakulima kwani huenda ikafichwa na tena kuuzwa mwaka ujao kwa bei ya juu.

[wp_radio_player]