‘MUGUMO’ WA POKOT MAGHARIBI WAANGUKA.


Baraza la wazee kaunti hii ya Pokot magharibi linatarajiwa kukutana kujadili chanzo cha kuanguka kwa mti wa kihistoria katika kaunti hii unaojulikana kama simotwo au mnagei.
Kulingana na mwenyekiti wa baraza hilo eneo la Pokot Kusini Mastayit Lokales, huenda kuanguka kwa mti huo kunaashiria jambo ambalo litabainika katika kikao hicho cha wazee hasa ikizingatiwa hamna ishara kuwa mti huo uliangushwa na upepo mkali.
Kulingana na Lokales, huo umehifadhiwa tangu miaka ya awali na ilikuwa marufuku kwa mtu yeyote kuukaribia, na hivyo chanzo ya kuanguka kwake kinasalia kitendawili ambacho kinahitaji uvumbuzi.
Amemtaka gavana John Lonyangapuo kuwakabidhi wazee hao ng’ombe ndume ambaye watahitaji kuchinjia eneo la tukio wakati wazee hao wakitafuta sababu ya kuanguka mti huo.