MTU MMOJA AULIWA CHESOGON KUFUATIA KISA CHA UVAMIZI

Na Benson Aswani
Mtu mmoja ameuliwa jana jioni kwa kupigwa risasi eneo la sirmaj chesogon mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet na wavamizi wanaoaminika kutoka kaunti jirani.
Kulingana na vyanzo vya habari jamaa huyo alikumbana na mauti yake wakati akitoka katika shughuli zake za kila siku baada ya kupigwa risasi na watu waliomwona kwa umbali bila ya ufahamu wake.
Inaaminika kuwa maujai hayo ni ya kulipiza kisasi baada ya kuuliwa mama mmoja na wanawe wawili eneo la Ngachar kaben huko Elgeyo marakwet.
Visa vya uvamizi vimeonekana kuongezeka eneo hilo katika siku za hivi karibuni licha ya mshirikishi wa serikali kanda ya rift valley George Natembeya kuzuru eneo la Cheptulel na kuwahakikishia wakazi kuwa serikali inaweka mikakati ya kuhakikisha visa hivyo vinakabiliwa.