MTU MMOJA AFARIKI HUKU SITA WAKIJERUHIWA KATIKA AJALI YA KARAS KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Mtu mmoja amethibitishwa kuiaga dunia baada ya kuhusika kwenye ajali iliyohusisha pikipiki mbili jana usiku eneo la Karas kaunti hii ya Pokot Magharibi.
Akithibitisha hayo daktari katika hospitali ya Kapenguria Jacob Nang’ole amesema ajali hiyo ilihusisha jumla ya watu saba, ambapo wanne wanaendelea kuhudumiwa katika hospitali hiyo huku wawili wakisafirishwa hadi hospitali ya rufaa mjini Eldoret baada ya kupata majeraha mabaya.
Aidha amesema hospitali hiyo inatafuta njia ya kuwapata wazazi wa wanafunzi ambao wanakisiwa kuhusika kwenye ajali hiyo kabla ya kuweka wazi taarifa kuwahusu ili kuzuia hali ya taharuki miongoni mwa wazazi.