MTOTO AMETELEKEZWA PAKUBWA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI; YASEMA LIONS.
Jamii haijafanya juhudi za kutosha katika kumshughulikia mtoto hasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Akizungumza katika maandalizi ya kuadhimisha siku ya mtoto wa kiafrika itakayoadhimishwa hiyo kesho jumatano, mwanachama wa lion kaunti hii ya Pokot magharibi Carolyne Menach amesema idadi kubwa ya watoto katika kaunti hii hawapati lishe bora hali ambayo imewafanya kutokua katika kimo inavyostahili.
Aidha Menach amesema mengi yanapasa kufanywa katika kaunti hii kuhusu maswala ya elimu kwa mtoto ambapo kulingana naye wazazi wengi hawajatilia maanani elimu kwa wanao huku wakiwahusisha katika shughuli ambazo zinawafanya kutoendelea na elimu.
Menach sasa anatoa wito kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi kutumia maadhimisho ya kesho katika kuhakikisha mtoto anashughulikiwa inavyopasa hasa walemavu kwa kuwatoa ili waweze kupata msaada kutoka mashirika mbali mbali.