MTIHANI WA KITAIFA KCSE KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YANGOA NANGA VYEMA MAENEO YOTE NCHINI YA POKOT

Mtihani wa kitaifa kwa kidato cha nne KCSE unaanza rasmi hii leo kote nchini siku chache tu baada ya kukamilika ule wa darasa la nane KCPE.
Hali ya usalama imeimarishwa katika vituo mbali mbali vya mitihani kuhakikisha kuwa shughuli hiyo inaendeshwa vyema hasa maeneo ya bonde la kerio ambako kumekuwa kukishuhudiwa utovu wa usalama wa mara kwa mara.
Wadau katika sekta ya elimu wamewahimiza watahiniwa wanaofanya mtihani huo kudumisha nidhamu na kuzingatia walichofunzwa na walimu wao, huku wakiwatahadharisha dhidi ya wanaodai kuuza mitihani hiyo.
Jared obiero ni mkurugenzi wa elimu eneo la bonde la ufa.
Jumla ya Wanafunzi alfu mianane thelathini na moja na kumi na watano wameratibiwa kuanza rasimi mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE leo hii jumatatu tarehe kumi na nne.
Mtihani huo utafanyika kwenye takribani vituo alfu kumi mianne kumi na vitatu kote nchini.
Baraza la mitihani ya kitaifa KNEC limesema kwamba idadi ya watahiniwa mwaka huu imeongezeka kwa Wanafunzi alfu sabini na nane na Arobaini na watatu sawa na asilimia tisa nukta nne.
Aidha imesema kwamba pana vituo mianne themanini na vitatu ambavyo mitihani itakuwa ikisambazwa kesho asubuhi watahiniwa wataanza na somo la kiingereza karatasi ya kwanza kisha kemia karatasi ya kwanza.
Aidha siku ya pili watafanya somo la hisabati na kiingereza ya ufahamu English composition.
Ikumbukwe kwamba baadhi ya masomo katika lugha ya kifaranza kijerumani na Arabia yalifanyika februari tarehe ishirini na nane.