MTIHANI WA KIDATO CHA NNE UMENGOA NANGA BILA TASHWISHI YEYOTE KWA MARA YA PILI KATIKA KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI

Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne kcse unatarajiwa kuendelea hii kwa siku ya pili baada ya kuanza rasimi hapo jana.
Leo hii watahiniwa wa kcse wanafanya somo la hisabati na karatasi ya pili ya kiingereza baada ya kufanya somo la kiingereza karatasi ya kwanza na kemia karatasi ya kwanza hapo jana
Usalama umeimarishwa hasa maeneo ambako kumekuwa kukishuhudiwa visa vya uvamizi wa mara kwa mara huku maafisa wa usalama wakitoa hakikisho la usalama wa kutosha na mazingira tulivu katika kipindi cha mtihani huo.
Naibu kamishina wa Kapenguria Elvis Korir ambaye alishuhudia ufunguzi wa makontena ya mitihani mapema leo amesema shughuli hiyo ilianza bila changamoto yoyote akisema kuwa hawatarajii visa vyovyote visivyo vya kawaida.
Kulingana na mkurugenzi wa elimu kaunti hii ya Pokot magharibi Fredrick kiiru jumla ya watahiniwa alfu 9993 wanafanya mtihani huo katika vituo 158 vya mitihani kauli iliyosisitizwa na mkurugenzi wa elimu eneo bunge la Kapenguria Charles manyara ambaye aidha amesema hamna kisa chocho cha mimba za mapema ambacho kimeripotiwa kufikia sasa.