MTIHANI WA DARASA LA NANE KCPE UMENGOA NANGA MAPEMA HII LEO KOTE KATIKA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Hatimaye mitihani ya kitaifa kwa darasa la nane KCPE inaanza rasmi hii leo kote nchini.
Mitihani hii inafanyika baada ya kuahirishwa kutokana na mabadiliko katika kalenda ya masomo ambayo ilitokana na athari za janga la corona.
Kulingana na mkurugenzi wa elimu eneo la kipkomo katika kaunti hii ya pokot magharibi Evans onyancha jumla ya wanafunzi alfu 2,550 wanatarajiwa kufanya mtihani huo mwaka huu eneo hilo idadi hii ikiwa juu ikilinganishwa na watahiniwa waliofanya mtihani huo mwaka jana.
Wakati uo huo Onyancha amesema kuwa visa vya mimba za mapema ambavyo huenda vitaripotiwa wakati wa mtihani huo ni vichache mno ikilinganishwa na awali kutokana na mikakati ambayo iliwekwa na wadau kuzuia hali hiyo.
Zaidi ya wanafunzi milioni moja elfu 225 mia sita sitini na tatu wa darasa la nane kote nchini wananatarajiwa kuanza rasmi mtihani wao wa kitaifa kcpe hii leo.
Mtihani huo utaandaliwa kwa siku tatu mfululizo na utakamilika siku ya jumatano huku ukiandaliwa katika vituo elfu 28, 248 nchini.
Hii leo watahiniwa wataanda na mtihani wa somo la hisabati saa mbili unusu asubuhi hadi saa nne unusu, kisha somo la kiingereza lugha kuanzia saa tano unusu na baadaya kutamatisha na mtihani wa insha ya kiingereza yaani cpomposition.
Katika kaunti ya baringo baadhi ya wanafunzi wamehamishiwa hadi kwenye vituo tofauti za mitihani kwa mfano wanafunzi wa shule ya msingi ya sinoni na kasiela watafanyia mitihani yao katika shule ya upili ya mochongoi.