MTAMBO WA SOLA ULIOIBWA WATAPATIKANA UMETUPWA NDANI YA SHULE YENYEWE

Siku moja tu baada ya kituo hiki kuangazia wizi wa mitambo miwili ya sola katika shule ya wasichana ya St Bakhita eneo bunge la kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi, mtambo mmoja umerejeshwa kwa shule hiyo.
Akithibitisha hayo mwenyekiti wa kamati ya miundo msingi katika shule hiyo Renson Apakamoi amesema mtambo huo ulirejeshwa hiyo jana huku akitoa wito kwa wale ambao walichukua mtambo mwingine kuurejesha.
Apakamoi ameonya kuwa watatumia kila mbinu kuhakikisha mtambo huo unapatikana iwapo mhusika wa wizi huo hatachukua hatua za kuurejesha
Hata hivyo amesema kuwa mtambo uliorejeshwa una alama za mipasuko hali anayosema kuwa huenda ilitokea katika harakati za kuuondoa sehemu ambayo ulikuwa umetundikwa japo akisema la muhimu ni kuwa umerejeshwa.