MSWADA WA MAREKBISHO YA KATIBA WA 2020 WAPIGIWA DEBE KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI


Viongozi mbalimbali nchini wameendelea kuupigia upato mswada wa marekebisho ya katiba wa 2020.
Akizungumza katika hafla ya kuchangisha pesa kwa makundi 43 ya akina mama mjini Ortum, Simon Kitalei Kachapin ambaye alikuwa gavana wa kwanza wa kaunti ya Pokot Magharibi amesema kuongezeka kwa mgao wa fedha kutoka asilimia 15 hadi asilimia 35 kutakuwa ni jambo la manufaa kubwa sana kwa wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi ambaye alikuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo ametaka wananchi kutohusisha mswada wa BBI na uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Mbunge wa Tiaty William Kamket kwa upande wake amemsifia Gideon Moi akisema kwamba tayari amekuwa na uhusiano mwema na viongozi wengi katika pembe zote za taifa la Kenya, hali itakayompa uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa Wakenya.